al-Fawzaan kuhusu al-Qaradhwaawiy na kitabu chake “al-Halaal wal-Haraam”

Ni jambo linalotambulika kuwa waislamu hii leo wanaishi katika majaribu makali kwa sababu ya mkondo wa magharibi na ustaarabu wenye sumu na tabia na desturi zinazopingana na hukumu nyingi za dini yetu. Kwa ajili hiyo ni lazima kwa waislamu wote kwa ujumla na khaswa wanazuoni wasimame kidete kwa ajili ya kuzuia mkondo huu mbaya dhidi ya dini yao na kuvunja shubuha. Lakini badala ya kuchukua msimamo huu mtukufu, tunawaona kwa masikitiko makubwa baadhi ya wanazuoni wetu na waandishi  wanakuwa ni wenye kueneza nyingi katika batili hizi zinazokuja na wanazitafutia mambo ya kuyatakasa ijapo ni kwa gharama ya dini. Matokeo yake wakawa ni wenye kutafuta maoni dhaifu na makosa ya wenye kujitahidi kwa ajili ya kutaka kuyaegemezea maoni yao.

Miongoni mwa waandishi hao ni mtunzi wa kitabu “al-Halaam wal-Haraam”. Kitabu chake kina sehemu kubwa ya mambo hayo. Nimezundua makosa yake katika kitabu hiki ambacho kwa sasa nakichapisha mara ya pili.

Mtunzi

1396-04-27/1976-04-26

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-I´laam bi Naqd Kitaab-il-Halaal wal-Haraam, uk. 3
  • Imechapishwa: 07/11/2022