Swali: Ipi nasaha zako kwa vijana wengi ambao wamejishughulisha sana kusambaza kanda za wapiga visa na watoa mawaidha na wanapuuza kusambaza kanda za kielimu?

Jibu: Wale wanaojishughulisha na kanda hizi, kanda za watoa mawaidha ambao mimi naona kuwa ni wenye kuwajengea madaraja Ahl-ul-Bid´ah na mapote… Ahl-ul-Bid´ah na mapote wanawajengea madaraja watu hawa. Wanawawinda vijana kwazo. Wanaanza kwa mawaidha, kulia na unyenyekevu. Wanajidhihirisha namna hii mbele ya vijana. Pindi vijana wanapojisikia salama na utulivu kwao, basi wanawawekea katika nafsi zao utata na wanawatuma kwa hao ambao wamewapa kazi hio ya kuwawinda hawa vijana. Kwa ajili hiyo utaona hawa watoa mawaidha wana mafungamano yenye nguvu ima na mapote potevu au makundi  yaliyoangamia. Humkuti Salafiy humo na wala hawana mafungamano na Salafiyyuun. Bali wanawachezea shere na hila Salafiyyuun na wanatahadharisha kufata mfumo wao. Wanasema wana msimamo mkali, ufidhuli na kadhalika. Na wanawasahilishia watu kutumbukia kwa watu wa Bid´ah.

Mimi ninawanasihi vijana wa ki-Salafiy kujishughulisha na elimu sahihi na mfumo wa Salaf sahihi. Ikiwa wanataka mawaidha, yapo katika Kitabu cha Allaah. Kama wanataka elimu ipo katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kama mlivyosikia katika Hadiyth ya al-´Irbaadhw wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anatoa mawaidha, basi nyoyo zinatetemeka na macho yanatiririka machozi. Na wakati mwingine walikuwa wakilia kwa sauti za juu. Atayesoma kwa mfano Riyaadh-us-Swaalihiyn ataona kuwa kuna yakutosheleza katika Sunnah za Mtume wa Allaah ili mtu asiwe na haja ya kuwasikiliza watu kama hawa. Na mawaidha yao unakuta yamejaa Bid´ah, ukhurafi na Hadiyth dhaifu na za kuundwa. Yote ni kwa kuwa hawa watoa mawaidha sio wanazuoni.

Salaf walikuwa wakiwadharau hawa wapiga visa, wakitahadharisha watu dhidi yao na uongo wao. Kwa masikitiko makubwa ni hivyo.

Kwa hali yoyote mfumo wa Salaf uko wazi. Tunawanasihi vijana kama kweli wanataka mawaidha na mafunzo, yapo ya kutosha katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Aliulizwa Abu Haatim kuhusu vitabu vya al-Haarith al-Muhaasibiy. Alikuwa ni mjuzi, mchaji Allaah na mwenye kuipa nyongo dunia zaidi kuliko watu hawa watoa mawaidha. Na alikuwa mbali zaidi na Bid´ah kuliko watu hawa. Kulipatikana katika vitabu vyake kitu kama Tasawwuf ambayo haiwezi kukosa katika mawaidha ya watu hawa. Aliulizwa Abu Zur´ah, imaam mkubwa na mtukufu wa Sunnah kuhusu vitabu vya al-Haarith. Akasema:

“Viacheni. Ni vitabu vya upotofu na Bid´ah.”

Wakasema vina mafunzo. Akasema:

“Yule ambaye hakupata mafunzo kwa Kitabu cha Allaah, hawezi kamwe kupata mafunzo kwa hivyo.”

Ndugu! Huu ndio mfumo wa Salaf! Walikuwa wakitahadharisha vitabu vya watu wa Bid´ah na mtu kuviangalia. Na walikuwa wakitahadharisha falsafa kwa kuwa ni Bid´ah na upotofu. Shikamaneni na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake na mfumo wa Salaf. Naapa kwa Allaah yule ambaye anamili kwa watu hawa mwishowe atakuja kupinda. Na mwenye kufaulu ni yule mwenye kupata mafunzo kwa makosa ya wengine. Chukueni mafunzo kwa vijana waliopotea waliokuwa juu ya mfumo wa Salaf. Mwisho wao uliishilia kuleta tafsiri mbovu na propaganda za batili mpaka hapo walikuja kuwa maadui wakubwa wa Ahl-us-Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=123813
  • Imechapishwa: 08/11/2022