al-Fawzaan kuhusu al-Halabiy na fatwa ya kitabu chake

Swali: Uliongelea kuhusu kujitokeza kwa Irjaa´. Na tumesikia kuwa al-Lajnah ad-Daaimah imejirejea ukosoaji wake dhidi ya kitabu cha al-Halabiy na Shukriy na kwamba al-Halabiy alifanya matembezi kwenye kamati na akabainisha kuwa kuna makosa kwenye hii fatwa. Je, hili ni kweli?

Jibu: Huu ni uongo mtupu. Kamati haikurejea wala haitorejea nyuma – Allaah akitaka – kutokamana na haki na kubainisha batili. Hakuna aliyetembelea kamati wala yeye hakuja kwenye kamati. Hata tukisema kuwa ameitembelea kamati. Ndio nini sasa? Kamati – Allaah akitaka – haitorejea nyuma kutokamana na haki hata siku moja. Bali yeye ndiye analazimika kujirejea kutokamana na na batili na atubu kwa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.albaidha.net/vb/showthread.php?p=94250
  • Imechapishwa: 13/11/2022