Maafikiano ya Tabdiy´ ni kanuni ya al-Halabiy

Swali: Je, ni sharti kuwepo maafikiano wakati wa kumzingatia fulani kuwa ni mzushi?

Jibu: Hapana. Hii ni kanuni iliyozuliwa. Ni moja miongoni mwa kanuni za al-Halabiy. Mwanachuoni akithibitisha dalili juu ya kwamba fulani ni mzushi na akathibitisha kuwa hoja imekwishamsimamia, ima kwa mahojiano au kupitia kitu ambacho kila mtu anajua kuwa ni Bid´ah, itatosha. Kusema kuwa ni lazima kuwepo maafikiano ni jambo halina msingi kwa Salaf.

Watu hawa wanachotaka ni kuwafanya Ahl-ul-Bid´ah wang´ae na wafiche aibu, kasoro na fedheha zao.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=128982
  • Imechapishwa: 13/11/2022