al-Albaaniy kuhusu kuchukua elimu kwa watu wa Bid´ah

Muulizaji: Ni sawa kutaja yale ambayo umeshaulizwa zaidi ya mara moja, nayo ni kustafidi kwa kuchukua elimu kutoka kwa kwa Ahl-ul-Bid´ah…

al-Albaaniy: Ndio, kuna watu wa Bid´ah ambao wana elimu katika kisomo cha Qur-aan, Tajwiyd, visomo, sarufi na misingi ya Fiqh au Hadiyth, hata kama hawafanyii kazi. Ikiwa karibuni hakuna Suuniy anayefuata Sunnah ambaye mtu anaweza kujifunza baadhi ya elimu hizi, inajuzu kuchukua elimu hii au ile kutoka kwao, lakini kwa sharti mtu awe na tahadhari na Bid´ah zao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (511)
  • Imechapishwa: 22/04/2015