Swali: Ni yapi maoni yenu kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh na kitabu chao “Tabliyghiy Niswaab”?

Jibu: Kuhusiana na kitabu, mimi sijakisoma.

Ama kuhusiana na sehemu ya kwanza, jibu langu limesajiliwa na kutolewa: Jamaa´at-ut-Tabliygh ni Suufiyyah wa zama hizi.

Jambo la kwanza Jamaa´at-ut-Tabliygh wanasema kwa kuweka wazi kwamba hawalinganii katika kusahihisha ´Aqiydah.

Jambo la pili hawatilii umuhimu kusafisha akili yao, fikira zao na maalumaat yanayohusiana na Uislamu katika Hadiyth dhaifu na Hadiyth zilizoundwa kama jinsi hawajali kuifasiri Qur-aan kwa mfumo wa Salaf. Wengi katika waliokuwa na wao walizuiawa kusahihisha makosa yao – hata kama yataelekea kwenye mzunguko wao wa karibu – sawa ikiwa yatahusiana na ´Aqiydah au Hadiyth.

Wao ni kama baadhi ya makundi, makundi yanayojulikana kwa kutotilia umuhimu juu ya masuala haya mawili. Ndugu zetu ambao wamechanganyika nao katika kulingania katika Uislamu, jambo ambalo linaonekana kuwa ni lizuri, walipoona kuwa wana upotevu huu wakawa wameachana nao.

Mmoja wao amenihadithia – alikuwa ni daktari Kuwait ambaye aliathirika na Salafiyyah – jinsi kila siku walivyokuwa wakianza kwa chumvi kabla ya kula. Akawauliza kuhusu sababu. Wakasema kwamba kuna Hadiyth ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuanza kwa chumvi kabla ya chakula, anakingwa na maradhi sabini.”

Wakati alipowaambia kwamba ni Hadiyth iliyoundwa na kwamba vitabu vyote vya Hadiyth vinaitia ila, wakasema:

“Namna hii ndivyo wanavyosema Mashaykh zetu.”

Hapa kunamalizikia tatizo likubwa ambalo linaweza kumithiliwa na shari yule aliyesema:

Bwana nyumbani akipiga dufu wakazi wa nyumba hawana jengine la kufanya zaidi ya kucheza

Hili ikiwa linatolea dalili juu ya kitu, basi linatolea dalili juu ya kwamba Mashaykh wa watu hawa hawatilii umuhimu kusoma Hadiyth na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (436)
  • Imechapishwa: 22/04/2015