Ahl-us-Sunnah wameafikiana ya kwamba uombezi ni kwa ajili ya waumini watenda madhambi

Swali: Je, watenda madhambi makubwa wa Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) watapata uombezi? Je, wataingia Peponi au hapana?

Jibu: Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya watenda madhambi makubwa zimethibiti na zimepokelewa kwa mapokezi mengi. Salaf katika Maswahabah, wale waliowafuata kwa wema na maimamu wa waislamu wameafikiana juu ya hilo. Waliozozana juu ya hilo ni Ahl-ul-Bid´ah katika Khawaarij, Mu´tazilah na wengineo.

Hakuna yeyote yule ambaye moyoni mwake alikuwa na imani kiasi ya mbegu ndogo kabisa atakayebaki Motoni. Bali wote watatoka Motoni na baadaye waingie Peponi.

Baada ya hapo Peponi kutabaki nafasi. Ndipo Allaah aumbe viumbe wengine na awaingize Peponi. Haya yamesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (4/309)
  • Imechapishwa: 20/03/2019