Du´aa ya bwanaharusi kabla ya kumwingilia mke aisome kimyakimya

Swali: Ni Sunnah ipi iliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati mume anapoingia kwa mke wake?

Jibu: Miongoni mwa Sunnah mtu amshike mwanzoni mwa kichwa chake na aseme:

اللّهُـمَّ  إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ خَيْـرَها، وَخَيْـرَ ما جَبَلْـتَهَـا عَلَـيْه، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّها، وَشَـرِّ ما جَبَلْـتَهَـا عَلَـيْه

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kheri yake na kheri ya maumbile Uliyomuumba  nayo na najilinda kwako kutokamana na shari yake na shari ya Uliyomuumba  nayo.”

Lakini asiyaseme maneno haya kwa sauti ya juu. Kwa sababu akiyasema kwa sauti yenye kusikika huenda mwanamke akamkimbia. Lakini amshike kichwani mwake kama vile kujifanya kama anataka kumbusu halafu ndio azungumze maneno haya. Haya ndio ninayoyajua kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusiana na hili.

Vilevile pale anapotaka kumwingilia basi ni lazima kumchezesha kwanza na kumpapasa mpaka na yeye mwanamke ashikwe na matamanio kama alivyoshikwa na yeye na matamanio.

Tatu wakati anapotaka kujamiiana naye basi aseme:

بسم الله، اللهم جنبنا الشيطان وجنب الشيطان ما رزقتنا

“Kwa jina la Allaah! Ee Allaah! Tulinde na shaytwaan na Ukilinde na shaytwaan kile ulichoturuzuku.”

Akisema hivo na Allaah akawakadiria kupata mtoto, basi kamwe kabisa shaytwaan hatomdhuru.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1059
  • Imechapishwa: 20/03/2019