161. Mwisho wa kitabu “Sharh Nawaaqidh-il-Islaam”

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Swalah na salamu zimwendee mbora wa viumbe; Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

MAELEZO

Shaykh-ul-Islaam amemalizia kijitabu hiki kwa kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Huku ni kumaliza kuzuri. Kumswalia Mtume ni jambo limewekwa katika Shari´ah mwanzoni wa kitendo na mwishoni mwake. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

”Hakika Allaah anamsifu na Malaika wake wanamuombea msamaha Mtume. Enyi walioamini msifuni na msalimieni kwa mamkizi yaliyojaa amani.” (al-Ahzaab 33:56)

Hii ni haki ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu yetu; kumsifu na kumsalimia.

Allaah kumswalia mja Wake maana yake ni kumsifu katika walimwengu wa walioko juu.

Malaika kumswalia mja maana yake ni kwamab wanamuomba msamaha.

Swalah ya wanadamu maana yake ni kuomba du´aa. Sisi tunaposema:

“Swalah na salamu zimwendee Mtume.”

maana yake ni kwamba tunamuomba Allaah amsifu kwa walimwengu walioko juu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 203-204
  • Imechapishwa: 20/03/2019