160. Midhali uko hai usijiaminishe nafsi yako

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Tunajikinga kwa Allaah dhidi ya yale yanayopelekea katika ghadhabu Zake na adhabu Yake iumizayo.

MAELEZO

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amemalizia kijitabu hiki kwa kuomba kinga, kushikamana na Allaah na kuomba kinga kwa Allaah kutokamana na ghadhabu Zake na sababu zinazopelekea katika ghadhabu Zake (Subhaanahu wa Ta´ala). Haya ni katika mambo ambayo yanamfanya muislamu kumuogopa Allaah (´Azza wa Jall) na kwamba asijiaminishe juu ya nafsi yake kutokamana na fitina na upotevu maadamu bado yuhai. Kwa ajili hii Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Yule anayetaka kuigiza basi awaigize wale ambao wameshakufa. Kwani hakika aliyehai hakuaminiwi juu yake fitina.”[1]

Aliyehai fitina haiaminiki juu yake hata kama atakuwa ni katika watu wenye kumcha Allaah zaidi na mjuzi zaidi. Maadamu bado yuhai basi kuna khatari akapatwa na fitina.

[1] Ameipokea al-Laalakaa-iy katika “Usuul-us-Sunnah” (130-131), ´Abdur-Razzaaq katika “Jaamiy´ Bayaan-il-´Ilm wa Fadhwlih (1881) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 203
  • Imechapishwa: 20/03/2019