Imaam al-Aajurriy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wanadhihirisha kuamrisha mema na kukataza maovu.” (ash-Shariy´ah (01/325)

Kama ilivyo hali ya Khawaarij leo. Wametilia nguvu kwa kiasi kikubwa katika kuamrisha mema na kukataza maovu, lakini hata hivyo Bid´ah kubwa sio maovu kwao. Bid´ah za shirki ambazo Ahl-us-Sunnah wamezitilia umuhimu zaidi kuliko maasi. Kwa sababu gani wametilia umuhimu Bid´ah? Kwa sababu mtu wa Bid´ah ni muovu zaidi kuliko mtawala mpotevu na ni muovu kuliko mtenda maasi. Kwa nini? Kwa kuwa huyu anaiharibu dini ya Allaah, anaibadili na anaiwaletea watu juu ya sura ya kwamba ndio dini ya Allaah. Tofauti na mtawala ambaye yeye atasema kuwa ameyachukua kutoka Ulaya au Amerika na hasemi kuwa ameyachukua kutoka kwa Allaah. Lakini watu hawa – watu wa Bid´ah – wanachosema ni kwamba dini yao ni kutoka kwa Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26874
  • Imechapishwa: 15/05/2015