Leo wanawachafua Ahl-us-Sunnah na kuwapa picha mbaya kwa matusi haya khabithi ambayo Khawaarij na Rawaafidhw hawakuwa wakiyatoa. Khawaarij leo na Rawaafidhw hawawaudhi Ahl-us-Sunnah kama wanavofanya watu hawa. Wamewarithi Khawaarij, Rawaafidhw na Murji-ah katika kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah. Wakati huo huo wao wenyewe wanajiita kuwa ni Ahl-us-Sunnah na Salafiyyuun. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba mfumo wa Sayyid Qutwub, al-Bannaa na al-Mawduudiy hauwi pamoja na mfumo wa Salaf. Kamwe! Upotevu na uongofu haviwi pamoja.

Fahamuni, enyi vijana! Shikamaneni na manhaj ya Salaf. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba Ummah hautotoka katika matatizo na udhalili isipokuwa kwa kurudi katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ufahamu wa Salaf, kuhusiana na masuala ya Khawaarij na masuala mengine.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26874
  • Imechapishwa: 07/05/2015