Alama za leo [za Khawaarij] ni alama zile zile za Dhul-Khuwayswirah na walio baada yake. Dhul-Khuwayswirah alimkosoa Mtume katika suala la [ugawaji] mali. Wafuasi wake waliotoka katika kizazi chake walimkosoa ´Aliy katika hukumu na mali. Khawaarij leo wameigeuza dini yote na kuikomeka katika Haakimiyyah. Wamesahau Tawhiyd kabisa na wamewasawazisha watu nayo. Wamewaghafilisha watu na shirki, uchawi, Bid´ah na upotevu na yanawaangamiza wengi katika wao na kuingia motoni na tunaomba kinga kwa Allaah. Hawahisi ´Aqiydah hii potevu ambayo Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam) waliipiga vita. Ndio ya kwanza waliyoanza nayo. Wametilia umuhimu Haakimiyyah peke yake. Wakiwapiga vita wanasekula na wengineo, hawawapigi vita kwa ajili ya jengine isipokuwa tu ni kwa ajili ya kushindishana kupata uongozi. Wanawapiga vita wapinzani wao kwa ajili ya kutafuta uongozi tu. Wanasekula wanachotafuta ni uongozi na wao wanachotaka ni uongozi. Wanakuwa wakali kwa wanasekula wanapowapiga vita kwa ajili ya uongozi. Wanapokubaliana, wanakuwa na umoja na kushirikiana pamoja na wanasekula, wakomunisti, manaswara na kila kundi. Huu ndio uhakika wao leo kwa masikitiko makubwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26874
  • Imechapishwa: 07/05/2015