Swali: Kuna mwanamke aliweka nadhiri ya kufunga siku sita za Shawwaal kila mwaka. Je, afunge nadhiri kwanza au alipe zile siku alizokula katika Ramadhaan kwa sababu ya hedhi au damu yake ya uzazi? Vipi endapo swawm ya siku sita za Shawwaal ingelikuwa ni ya kujitolea kwanza; angelitakiwa kulipa deni la Ramadhaan kwanza au angelifunga swawm ya kujitolea?

Jibu: Bora ni yeye kutanguliza deni kisha baadaye ndio afunge siku sita. Ni mamoja siku sita hizo ni nadhiri au swawm ya kujitolea. Akamilishe Ramadhaan kwanza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/10481/تقديم-قضاء-صوم-رمضان-على-صوم-النذر-والتطوع
  • Imechapishwa: 18/03/2023