Swali: Je, mwenye kufa ndani ya Ramadhaan, siku ya ijumaa au katika usiku wa kuamkia ijumaa kifo chake kina ubora ukilinganisha na siku nyenginezo? Tumeyasikia hayo kutoka kwa baadhi ya ndugu.

Jibu: Sijui chochote juu ya hayo. Nasema kwamba sijui jambo hilo. Hadiyth zilizopokelewa kuhusu kufa siku ya ijumaa zote sio Swahiyh. Vivyo hivyo akifa ndani ya Ramadhaan sijui chochote kinachofahamisha juu ya fadhilah zake maalum. Hata hivyo kuna matarajio juu yake ya kheri kubwa endapo atakufa ilihali amefunga na ni mtu mwenye msimamo wa dini. Lakini sijui kitu chochote maalum kinachozungumzia kuhusu kufa ndani ya Ramadhaan. Kuhusu kufa usiku wa kuamkia ijumaa au siku ya ijumaa kumesimuliwa mapokezi yasiyokuwa Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12591/هل-الموت-في-يوم-الجمعة-او-رمضان-له-فضل
  • Imechapishwa: 18/03/2023