Aayah inayowazungumzisha watenda madhambi

Swali: Maana ya maneno Yake (Ta´ala):

قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ لا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعاً إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ

“Sema: “Enyi waja Wangu ambao mmepindukia juu ya nasfi zenu: “Msikate tamaa na rehema za Allaah. Kwani hakika anasamehe madhambi yote. Kwani hakika Yeye ni mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

Jibu: Wanazuoni wote wanaona kuwa inawahusu wenye kutubia, kwa sababu amesema:

لا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعاً

“… msikate tamaa na rehema za Allaah. Kwani hakika anasamehe madhambi yote.”

Hii inakusanya shirki na madhambi mengine. Hakubagua shirki. Kunaingia shirki na madhambi mengine. Kwa ajili hiyo wanazuoni wamesema kuwa inawahusu watubiaji.

Kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakikaha hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae.”[2]

Maana yake ni kwa wale ambao wamekufa kabla ya kutubia.

Aayah ya kwamba inawahusu wenye kutubia, kwa sababu Allaah amejumuisha na amesema kwa kuachia pasi na kumbagua yeyote. Dalili ya hilo ni kwamba ameachia na hakubagua shirki. Shirki haisamehewi kwa yule ambaye amekufa juu yake. Kisha akawaamrisha kurejea kwa maana kutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hiyo ndio maana ya msikate tamaa kwa msemo mwingine rejeeni kwa Allaah.

[1] 39:53

[2] 04:48

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24097/هل-تعم-قل-يا-عبادي-الذين-اسرفوا-كل-تاىب
  • Imechapishwa: 29/08/2024