Anayevaa hariri duniani hatoivaa Aakhirah?

Swali: Anayevaa hariri duniani hatoivaa Aakhirah?

Jibu: Ni kwa njia ya matishio na makemeo kwa mujibu wa Ahl-us-Sunnah. Kwa sababu wakazi wa Peponi mavazi yao ni hariri. Udhahiri wake ni kwamba watazuiwa kuingia Peponi. Kwa hivyo ni kwa njia ya makemeo. Ni kama mfano wa Hadiyth isemayo:

“Hatoingia Peponi mwenye kueneza uvumi.”

Ni kwa njia ya matishio ili watu watahadhari na dhambi hii. Allaah akimkubalia tawbah yake na kusamehe ataingia Peponi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24099/معنى-من-لبس-الحرير-لم-يلبسه-في-الاخرة
  • Imechapishwa: 29/08/2024