Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
2 – ´Ammaar bin Yaasir (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule atakayefunga siku ya shaka basi kwa hakika amemuasi Abul-Qaasim (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam).”[1]
al-Bukhaariy ameitaja hali ya kuwa na cheni ya wapokezi pungufu, watano wameiunganisha na ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan.
Haafidhw Ibn Hajar amesema:
”Kuna kasoro iliyofichika katika Hadiyth ambayo imetajwa. at-Tirmidhiy katika “al-´Ilal” ya baadhi ya wapokezi wamesema juu yake: Kwa kutoka kwa Ibn Ishaaq ambaye amesema: ”Nimehadithiwa kutoka kwa Swilah.”[2]
Hata hivyo kile kinachofahamishwa na Hadiyth juu ya makatazo ya kufunga siku ya shaka kimepokelewa na jopo la Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), ikiwa ni pamoja na Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) inayokataza kufunga siku kadhaa kabla ya Ramadhaan.
Hadiyth ni dalili ya uharamu wa kufunga siku ya shaka, kwa sababu kufunga siku hiyo ni kumwasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hadiyth hii ina hukumu ya kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwani ´Ammaar (Radhiya Allaahu ´anh) hangeweza kutoa hukumu hii isipokuwa ni kwa sababu alikuwa na elimu kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Pia ni kwamba inatiwa nguvu na Hadiyth zinazokataza kuipokea Ramadhaan kwa kufunga kabla yake na zile zinazoamrisha kufunga kwa kuona mwezi mwandamo.
[1] al-Bukhaariy (27/3), Abu Daawuud (2334), at-Tirmidhiy (686), an-Nasaa’iy (2188), Ibn Maajah (1645), Ibn Khuzaymah (1914) na Ibn Hibbaan (3594).
[2] Taghliyq-ut-Ta´liyq (04/141).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/9-10)
- Imechapishwa: 29/01/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
148. Yeyote anayejifananisha na watu basi ni katika wao
3 – ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: ”Nimetumilizwa kabla ya kusimama Saa kwa upanga mpaka aabudiwe Allaah hali ya kuwa ni Mmoja – asiyekuwa na mshirika. Riziki yangu imefanywa ni kutoka chini ya kivuli cha mkuki wangu, unyonge…
In "7. Sharti ya saba ya jilbaab"
01. Hadiyth “Msiitangulizie Ramadhaan kwa kufunga siku moja au mbili… “
Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema: 669- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Msiitangulizie Ramadhaan kwa kufunga siku moja au mbili, isipokuwa mtu ambaye alikuwa akifunga swawm. Basi aiendeleze.”[1] Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim. 670- ´Ammaar bin Yaasir (Radhiya Allaahu…
In "Mukhtaswar-uz-Zabiyd"
Fadhilah za kufunga siku ya ´Arafah
1 – Abu Qataadah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: ”Inafuta dhambi za mwaka wa kabla yake na mingineyo.”[1] Ameipokea Muslim, tamko ni lake, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, Ibn Maajah na at-Tirmidhiy ambaye tamko lake linasema: “ Swawm ya siku ya ´Arafah; hakika…
In "Swawm katika Dhul-Hijjah"