Kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi `siku ya kwanza` ni siku ya tarehe 30 ya Sha´baan pale ambapo mawingu, ukungu au kitu kinginecho kinazuia kuonekana mwezi mwandamo. Siku hii haipaswi kufungwa, kwa mujibu wa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ikiwa mtafunikwa, basi kamilisheni idadi ya Sha´baan kuwa siku thelathini.”[1]
Hii ni dalili ya wazi ya kwamba siku ya tarehe 30 haitakiwi kufungwa, kwa sababu msingi ni kuendelea kuwepo kwa Sha´baan hadi uthibitisho wa uhakika kwamba Ramadhaan imeingia.
Wale wanaotofautisha kati ya hali ya mawingu na anga safi kwa kusema kwamba kufunga kunahitajika kama kuna mawingu, lakini si kama anga ni safi, hawako sahihi. Hayo ndio maoni ya Hanaabilah na ndio yenye kuelezwa katika vitabu vyao vingi. Dalili yao ni kitendo cha Ibn ´Umar, kama itavyoelezwa – Allaah akitaka.
[1] al-Bukhaariy (1909).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/10)
- Imechapishwa: 29/01/2025
Kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi `siku ya kwanza` ni siku ya tarehe 30 ya Sha´baan pale ambapo mawingu, ukungu au kitu kinginecho kinazuia kuonekana mwezi mwandamo. Siku hii haipaswi kufungwa, kwa mujibu wa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ikiwa mtafunikwa, basi kamilisheni idadi ya Sha´baan kuwa siku thelathini.”[1]
Hii ni dalili ya wazi ya kwamba siku ya tarehe 30 haitakiwi kufungwa, kwa sababu msingi ni kuendelea kuwepo kwa Sha´baan hadi uthibitisho wa uhakika kwamba Ramadhaan imeingia.
Wale wanaotofautisha kati ya hali ya mawingu na anga safi kwa kusema kwamba kufunga kunahitajika kama kuna mawingu, lakini si kama anga ni safi, hawako sahihi. Hayo ndio maoni ya Hanaabilah na ndio yenye kuelezwa katika vitabu vyao vingi. Dalili yao ni kitendo cha Ibn ´Umar, kama itavyoelezwa – Allaah akitaka.
[1] al-Bukhaariy (1909).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/10)
Imechapishwa: 29/01/2025
https://firqatunnajia.com/07-makusudio-ya-siku-ya-shaka/