Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

2 – ´Ammaar bin Yaasir (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayefunga siku ya shaka basi kwa hakika amemuasi Abul-Qaasim (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam).”[1]

al-Bukhaariy ameitaja hali ya kuwa na cheni ya wapokezi pungufu, watano  wameiunganisha na ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan.

Haafidhw Ibn Hajar amesema:

”Kuna kasoro iliyofichika katika Hadiyth ambayo imetajwa. at-Tirmidhiy katika “al-´Ilal” ya baadhi ya wapokezi wamesema juu yake: Kwa kutoka kwa Ibn Ishaaq ambaye amesema: ”Nimehadithiwa kutoka kwa Swilah.”[2]

Hata hivyo kile kinachofahamishwa na Hadiyth juu ya makatazo ya kufunga siku ya shaka kimepokelewa na jopo la Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), ikiwa ni pamoja na Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) inayokataza kufunga siku kadhaa kabla ya Ramadhaan.

Hadiyth ni dalili ya uharamu wa kufunga siku ya shaka, kwa sababu kufunga siku hiyo ni kumwasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hadiyth hii ina hukumu ya kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwani ´Ammaar (Radhiya Allaahu ´anh) hangeweza kutoa hukumu hii isipokuwa ni kwa sababu alikuwa na elimu kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Pia ni kwamba inatiwa nguvu na Hadiyth zinazokataza kuipokea Ramadhaan kwa kufunga kabla yake na zile zinazoamrisha kufunga kwa kuona mwezi mwandamo.

[1] al-Bukhaariy (27/3), Abu Daawuud (2334), at-Tirmidhiy (686), an-Nasaa’iy (2188), Ibn Maajah (1645), Ibn Khuzaymah (1914) na Ibn Hibbaan (3594).

[2] Taghliyq-ut-Ta´liyq (04/141).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/9-10)
  • Imechapishwa: 29/01/2025