98. Imani kwa mtazamo wa Murji-ah al-Fuqahaa´ na Ashaa´irah na Radd juu yao

Wala imani sio kuamini ndani ya moyo na kutamka kwa ulimi peke yake, kama linavyosema kundi katika Murji-ah. Nao si wengine ni Murji-ah al-Fuqahaa´. Wanasema kuwa imani ni kutamka kwa ulimi na kuamini ndani ya moyo ijapokuwa mtu hakufanya matendo. Hawayaingizi matendo ndani ya imani. Wameleta mambo mawili na wakaacha jambo la tatu. Wamesema kuwa matendo si jambo la lazima midhali mtu anatamka na anaamini. Wanaona kuwa mambo hayo yanatosha. Madhehebu haya ni batili pia. Ni lazima mtu afanye matendo. Allaah siku zote anaambatanisha imani na matendo:

آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ

“Wale walioamini na wakatenda mema.”[1]

Hakusema kuwa wameamini peke yake. Bali amesema:

آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ

“Wale walioamini na wakatenda mema.”

Imani haipatikani bila ya matendo. Irjaa´ ni madhehebu batili kwa vigawanyo vyake vyote.

Ashaa´irah wameleta vitu viwili na wakaacha kimoja. Wamesema kuwa imani ni kusadikisha kwa moyo ijapokuwa mtu hakutamka kwa ulimi wake. Mwenye kusadikisha kwa moyo wake ni muumini hata kama hakutamka.

[1] 48:29

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 136
  • Imechapishwa: 01/06/2021