95 – Zayd bin Aslam amesema:

”Ibn ´Umar alipita karibu na mchungaji akasema: ”Je, kuna kondoo anayefaa?” Akasema: ”Mmiliki wake hayuko hapa.” Ibn ´Umar akasema: ”Utamweleza kuwa ameliwa na mbwa mwitu.” Bwana akainua macho yake mbinguni na kusema: ”Allaah yuko wapi?” Ndipo Ibn ´Umar akasema: ”Naapa kwa Allaah! Mimi ndiye nina haki zaidi ya kukuuliza swali hilo.” Ndipo akamnunua yule mchungaji na kondoo, na baadaye akamwacha huru na akampa kondoo yule.”[1]

[1] Mtunzi ameisimulia katika asili kupitia kwa Abu Musw´ab az-Zuhriy: ´Abdullaah bin al-Haarith al-Jamhiy ametuhadithia: Zayd bin Aslam ametuhadithia… Cheni ya wapokezi hii ni nzuri. Mbali na ´Abdullaah bin al-Haarith al-Jamhiy al-Haatwibiy, ambaye ameelezwa katika  “Taqriyb-ut-Taqriyb” kuwa ni mkweli, wapokezi wake wengine wote ni madhubuti na ni wanaume wa al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 117
  • Imechapishwa: 12/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy