Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Kadhalika haitoshi pia kwa mwanamke kujifunika na kujisitiri kwa vazi halijitofautishi na vazi la wanaume. Bali kutofautisha kati ya vazi la mwanamke na mwanaume ni lengo pia. Ikiwa wanaume na wanawake wataamua kujisitiri kwa njia ya kwamba mavazi yao yakafanana, basi wangelikatazwa kutokana na hayo. Allaah (Ta´ala) amebainisha lengo hili pale aliposema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاء الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ذَلِكَ أَدْنَى أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

“Ee Nabii! Waambie wake zako na mabinti zako – na wanawake wa waumini – wajiteremshie Jilbaab zao; hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane wasiudhiwe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

Amezindua pia kwamba lengo ni ili mwanamke aweze kutambulika kupitia vazi lake. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

”Allaah amewalaani wanawake wenye kujifananisha na wanaume na wanaume wenye kujifananisha na wanawake.”

Amefungamanisha hukumu na jambo la kujifananisha na kwamba kila mmoja katika wao amejifananisha na sifa za mwengine. Kanuni hii nimeipambanua katika ”Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalafatu Asw-haab-il-Jahiym”.”[2]

[1] 33:59

[2] al-Kawaakib (93/132-134) ya Ibn ´Urwah al-Hanbaliy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 157-158
  • Imechapishwa: 24/10/2023