Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Jambo lililo wazi zaidi ni kwamba lengo la mavazi ya walipa kodi ya kulindwa ni kujitofautisha na waislamu ili kila kundi katika wao litendewe hukumu za dhahiri zinazonasibiana nalo, jambo ambalo linaweza kufikiwa kwa vazi lolote ambalo kundi husika linatambulika kwalo. Licha ya hivo huzingatiwa pia mambo ambayo ni mahususi zaidi. Kwa mfano vazi jeupe ni bora zaidi kuliko jingine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Lazimianeni na weupe. Wavisheni waliohai wenu na wavisheni sanda wafu wenu.”

Kwa hivyo si katika Sunnah kufanya mavazi ya walipa kodi ya ulinzi yakawa meupe na mavazi ya waislamu kuwa yenye rangi. Bali mambo ni kinyume na hivo. Vivyo hivyo katika unyoaji na mengineyo. Vivyo hivyo kuhusu mavazi ya wanaume na wanawake. Makusudio sio kujitofautisha peke yake – bali ni lazima kuzingatia kipengele cha kujifunika na kujisitiri.”[1]

[1] al-Kawaakib (93/132-134) ya Ibn ´Urwah al-Hanbaliy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 157-158
  • Imechapishwa: 24/10/2023