01. Hadiyth “Watu aina tatu hawasogelewi na Malaika… “

173 – ´Ammaar bin Yaasir (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu aina tatu hawasogelewi na Malaika; mzoga wa kafiri, mwanamme ambaye amejitia manukato yaliyokuwa na zafarani na mwenye janaba mpaka atawadhe.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud kupitia kwa al-Hasan bin Abiy-Hasan, kutoka kwa ´Amamar, licha ya kuwa hakusikia kutoka kwake[2].

Makusudio ya Malaika hapa ni wale wanaoteremka na rehema na baraka, na si wale wanaoandika matendo ya mtu; kwani wao hawatengani na mwanadamu kwa hali yoyote. Aidha imesemwa kwamba Hadiyth hii inamuhusu yule ambaye atachelewesha kuoga pasi na udhuru au akawa na uwezo wa kutawadha lakini pamoja na hivyo asifanye hivo. Vilevile imesemwa kwamba Hadiyth hii inamkusudia yule ambaye atachelewesha kuoga kwa kuzembea na kwa uvivu na akachukulia jambo hilo ndio mazowea yake.

[1] Nzuri kupitia zengine.

[2] Lakini imepokelewa kupitia njia zengine mbili zinazoitia nguvu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/184)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy