08. Hadiyth “Yule ambaye anamwamini Allaah na siku ya mwisho basi asiingie bafu za nje… “

172 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye anamwamini Allaah na siku ya mwisho basi asiingie bafu za nje isipokuwa awe na shuka ya juu. Yule ambaye anamwamini Allaah na siku ya mwisho basi asimwache mkewe kuingia katika bafu za nje. Yule ambaye anamwamini Allaah na siku ya mwisho basi asinywe pombe. Yule ambaye anamwamini Allaah na siku ya Mwisho basi asiketi kwenye meza kunakohudumiwa pombe. Yule ambaye anamwamini Allaah na siku ya Mwisho basi asikae chemba na mwanamke ambapo hakuna Mahram kati yake yeye na mwanamke huyo.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr”.

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/183)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy