07. Hadiyth “Mwanamke yeyote atakayevua nguo zake… “

171 – Ahmad, Abu Ya´laa, at-Twabaraaniy na al-Haakim wamepokea kupitia kwa Darraaj Abus-Samh, kutoka kwa as-Saa-ib ambaye amesema:

“Kikosi cha wanawake kiliingia kwa Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambapo akasema: “Nyinyi ni kina nani?” Wakasema: “Tunatoka kwa watu wa Himsw.” Akasema: “Kwa wale watu walio na bafu za nje?” Wakasema: “Kwani zina neno?” Akasema: “Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Mwanamke yeyote atakayevua nguo zake katika nyumba isiyokuwa yake,  basi Allaah ataivunja sitara kutoka kwake.”[1]

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/183)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy