06. Hadiyth “Kikosi cha wanawake kutoka Himsw… “

170 – Abul-Maliyh al-Hudhaliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Kikosi cha wanawake kutoka Himsw, kutoka Shaam, waliingia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambapo akasema: “Nyinyi ndio ambao wanawake zenu huingia katika bafu za nje? Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Hakuna mwanamke yeyote atakayevua nguo zake katika nyumba isiyokuwa ya mume wake isipokuwa atakuwa amevunja sitara ilioko kati yake yeye na Mola wake.”[1]

Ameipokea at-Tirmidhiy na tamko ni lake na akasema kuwa Hadiyth ni nzuri, Abu Daawuud, Ibn Maajah na al-Haakim ambaye amesema:

“Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/182-183)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy