05. Hadiyth “Siku moja wakati nilipokuwa natoka katika bafu za nje… “

169 – Umm-ud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Siku moja wakati nilipokuwa natoka katika bafu za nje nilikutana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye akasema: “Umetokea za wapi, ee Umm-ud-Dardaa´?” Nikasema: “Natokea bafu za nje.” Ndipo akasema: “Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake kwamba hakuna mwanamke yeyote ambaye atavua nguo zake kusikokuwa katika nyumba ya mmoja katika mama zake, isipokuwa amevunja sitara ilioko kati yake na kati ya Mwingi wa huruma.”

Ameipokea Ahmad na at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” kwa cheni za wapokezi ambao  ni wapokezi wa Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/181-182)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy