04. Hadiyth “Yule ambaye anamwamini Allaah na siku ya Mwisho basi asiketi kwenye meza… “

167 – ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye anamwamini Allaah na siku ya Mwisho basi asiketi kwenye meza kunakohudumiwa pombe. Yule ambaye anamwamini Allaah na siku ya Mwisho basi asiingie bafu za nje isipokuwa awe na shuka ya juu. Yule ambaye anamwamini Allaah na siku ya mwisho basi asimwache mkewe kuingia katika bafu za nje.”[1]

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/181)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy