Maneno yake:

“Ni mamoja ni wema au waovu.”

Kama tulivyotangulia kusema si sharti mtawala wa waislamu awe mwema mia kwa mia kama wale makhaliyfah waongofu. Bali ni lazima kuwatii hata kama watakuwa na kitu katika madhambi ambayo hayajafikia kiwango cha ukafiri na kutoka nje ya dini. Kuharibika kwake ni juu yake. Lakini ungozi wake ni kwa ajili ya manufaa ya waislamu.

Wakati  baadhi ya maimamu walipoulizwa ni nani anayesilihi zaidi kuwa imamu kati ya mtawala mwema lakini ni mdhaifu na mtawala mwingine ni mtenda madhambi lakini ni mwenye nguvu. Wakajibu kwamba yule mtenda madhambi. Kwa sababu wema na mdhaifu wema wake ni juu ya nafsi yake mwenyewe na udhaifu wake unawadhuru waislamu. Mtawala mtenda madhambi madhambi hayo ni juu ya nafsi yake na nguvu zake ni kwa waislamu.

Maneno yake:

“Ni mamoja ni wema au waovu.”

Haya ni tofauti na Khawaarij na Mu´tazilah ambao wanawafanyia uasi watawala waovu. Watawala waovu hapa kunakusudiwa wale watenda madhambi.

Maneno yake:

“Muda wa kuwa hawajaamrisha kumuasi Allaah.”

Ni lazima kuwatii. Wakiamrisha maasi:

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”[1]

Lakini ahadi yao haivuliki wakiamrisha maasi. Hatutowatii katika hili. Lakini itaendelea jambo la kuwatii katika mema na si katika mambo ambayo ni maasi. Tutawakhalifu katika maasi na tutawatii katika wema.

[1] Ahmad katika ”al-Musnad” (01/131 nambari. 1095) kupitia kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Pia imepokelewa kupitia kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) (01/409 nambari. 3889). Pia imepokelewa kupitia kwa ´Imraan bin Huswayn (Radhiya Allaahu ´anh) (05/66 nambari. 20653).  Muslim (1840), Abu Daawuud (2625) kupitia kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) kwa tamko lisemalo:

”Hakuna utiifu katika kumuasi Allaah.”

Katika kisa cha kikosi ambacho kiongozi wao aliwaamrisha kuingia ndani ya moto.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 128-129
  • Imechapishwa: 31/05/2021