Wakazi wa Peponi ni kila muumini na mwenye kumcha Allaah. Kwa sababu ndio wapenzi wa Allaah. Amesema (Ta´ala) kuhusu Pepo:
أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ
“Imeandaliwa kwa wenye kumcha Allaah.”[1]
أُعِدَّتْ لِلَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ
“… imeandaliwa kwa wale waliomwamini Allaah na Mitume Yake.”[2]
Wakazi wa Moto ni kila kafiri mla maangamivu. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu Moto:
أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ
”Umeandaliwa kwa makafiri.”[3]
فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ
“Ama wale walio mashakani, basi watakuwa Motoni.”[4]
[1] 03:133
[2] 57:21
[3] 02:24
[4] 11:106
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 133
- Imechapishwa: 12/12/2022