85. Tafsiri inayobainisha maana ya shahaadah ya kwanza

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Tafsiri inayoweka wazi haya, ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

“Pindi Ibraahiym alipomwambia baba yake na watu wake: “Hakika mimi najitenga mbali na yale mnayoyaabudu, isipokuwa Yule aliyeniumba, basi hakika Yeye Ataniongoa! Na akalifanya neno hili kuwa ni lenye kubakia katika kizazi chake ili wapate kurejea.”[1]

MAELEZO

Kitu bora kinachoweza kuifasiri Qur-aan ni Qur-aan yenyewe. Allaah amefasiri maana ya shahaadah ndani ya Qur-aan pale ambapo Allaah alisema kuwa Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

إِنَّنِي بَرَاءٌ

 “Hakika mimi najitenga mbali… “

Haya ni makanusho.

إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِ

“… isipokuwa Yule aliyeniumba… “

Bi maana isipokuwa Allaah. Haya ni mathibitisho. Aayah hii inathibitisha maana ya shahaadah kikamilifu.

[1] 43:26-28

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 169
  • Imechapishwa: 07/01/2021