84. Maana sahihi ya shahaadah ya kwanza kwa mujibu wa Qur-aan

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Maana yake ni kwamba hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah. “Hapana mungu” ni kukanusha kila kinachoabudiwa badala ya Allaah, wakati “isipokuwa Allaah” ni kuthibitisha ya kwamba ´ibaadah afanyiwa Allaah pekee. Hana mshirika katika ´ibaadah Yake, kama ambavyo hana mshirika katika ufalma Wake.

MAELEZO

Maana yake ni kwamba hapana mwenye kuabudiwa… – Hii ndio maana ya shahaadah. Si kama wanavosema wapotevu kwamba maana yake ni hapana muumbaji wala mwenye kuruzuku isipokuwa Allaah. Hii ni Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ambayo wanaikubali washirikina. Isitoshi wao hawasemi ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah`. Amesema (Ta´ala):

إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ

“Hakika wao walipokuwa wakiambiwa ´hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah` hufanya kiburi na wanasema: “Je, hivi kweli sisi tuache waabudiwa wetu kwa ajili ya mshairi mwendawazimu?”[1]

Waungu wetu bi maana waabudia wetu.

لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ

“… kwa ajili ya mshairi mwendawazimu?”

Wakimkusudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Walimsifu kwa mashairi na wendawazimu kwa sababu aliwaambia watamka ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` na baada ya kuwakataza kuyaabudu masanamu.

Isitoshe alipowaambia waseme ´hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaha` walisema:

أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ

“Amewafanya waungu kuwa ni mungu Mmoja?  Hakika hili ni jambo la ajabu mno!”[2]

Wanazingatia waungu wengi. Kwa hiyo ni dalili inayoonyesha kuwa maana yake ni hapana mwabudiwa wa haki asiyekuwa Allaah. Ingelikuwa maana yake ni hapana muumbaji wala mruzukaji mwengine asiyekuwa Allaah ni kitu wanachokikubali na wala hawazozani kwacho. Kama hiyo ndio ingelikuwa maana yake basi wasingekataa kutamka ´hapana mungu wa haki asiyekuwa Allaah`. Kwa sababu walikuwa wanapoulizwa ni nani aliyeumba mbingu na ardhi wakisema kuwa ni Allaah. Wanapoulizwa ni nani mwenye kuumba, ni nani mwenye kuruzuku, ni nani mwenye kuhuisha na mwenye kufisha wanajibu kwamba ni Allaah. Walikuwa ni wenye kukubali jambo hilo. Lau hiyo ingekuwa ndio maana ya “hapana mungu isipokuwa Allaah” basi wangekubali. Lakini maana yake ni kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah.

Iwapo utasema kuwa hapana mwabudiwa mwengine asiyekuwa Allaah ni kosa kubwa. Hiyo itakuwa na maana kwamba waabudiwa wote ni wa Allaah – Allaah ametakasika kutokamana na haya. Lau ukifungamanisha na “kwa haki” basi wanaondoka waabudiwa wote isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa hiyo ni lazima useme ´hapana mwabudiwa wa haki`. Kisha akabainisha kwa mujibu wa matamshi yake.

Hapana mungu –  Ni kukanusha kila kinachoabudiwa badala ya Allaah.

Isipokuwa Allaah – Ni kuthibitisha ´ibaadah kwa Allaah pekee hali ya kuwa yupekee hana mshirika.

Kwa hiyo hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah ndani yake mna ukanushaji na uthibititishaji. Tawhiyd ni lazima iwe na ukanushaji na uthibitishaji. Haitoshi kuthibitisha peke yake kama ambavo haitoshi kukanusha peke yake. Bali ni lazima kukanusha na kuthibitisha. Amesema (Ta´ala):

فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ

“Basi atakayemkanusha twaaghuut na akamwamini Allaah… ”[3]

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا

“Mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe Yeye na chochote.”[4]

Iwapo utasema “hapana mungu wa haki” haitoshi. al-Laat, al-´Uzzaa, Manaat na masanamu mengine yote yanaitwa waungu. Ni lazima useme hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Ni lazima kukusanya kati ya kukanusha na kuthibitisha mpaka ihakikike Tawhiyd na itokomezwe shirki.

[1] 37:35-36

[2] 38:05

[3] 02:256

[4] 04:36

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 166-169
  • Imechapishwa: 07/01/2021