84. ´Aqiydah ya Ibn ´Abdil-Wahhaab juu ya Jihaad na swalah nyuma ya viongozi

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Naona Jihaad ni yenye kuendelea pamoja na kila kiongozi. Ni mamoja ni mwema au muovu. Inafaa kuswali swalah ya mkusanyiko nyuma yao.

MAELEZO

Jihaad ni kutumia juhudi katika kupambana na makafiri kwa ajili ya kulinyanyua neno la Allaah. Lengo la Jihaad ni kulinyanyua neno la Allaah, kueneza Tawhiyd na kutokomeza shirki. Kwa sababu dini ya Allaah (´Azza wa Jall). Amesema (Ta´ala):

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

“Sikuumba majini na watu isipokuwa waniabudu.”[1]

´Ibaadah ni haki ya Allaah. Mwenye kumwomba badala ya Allaah analinganiwa kurejea katika Uislamu, kutubia na kuitakasa Tawhiyd. Akikataa anapigwa vita. Kwa sababu Allah amemtumiliza Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuja kulingania na kupambana. Kitu cha kwanza alinganie kisha Jihaad ije baada ya hapo ili kufuru isienee. Amesema (Ta´ala):

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لاَ تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلّهِ

“Piganeni nao mpaka kusiweko shirki na dini yote iwe kwa ajili ya Allaah pekee.”[2]

Katika Aayah nyingine:

وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّـهِ

”… na dini yote iwe kwa ajili ya Allaah.”[3]

Maneno Yake:

حَتَّى لاَ تَكُونَ فِتْنَةٌوَيَكُونَ الدِّينُ لِلّهِ

“… mpaka kusiweko shirki.”

bi maana shirki.

Maneno Yake:

وَيَكُونَ الدِّينُ لِلّهِ

“… na dini yote iwe kwa ajili ya Allaah pekee.”

bi maana asiabudiwe kiumbe yeyote. Bali aabudiwe Muumba (Subhaanahu wa Ta´ala).

Hili ndio lengo la Jihaad; kueneza Tawhiyd na kutokomeza shirki juu ya aradhi. Kwa sababu Allaah amewaumba viumbe ili wamwabudu Yeye. Wakimwabudu mwengine ima watubu na warejee au wapigwe vita. Kwani wakiachwa ukafiri utaenea. Kwa sababu makafiri wanaita katika ukafiri. Kafiri anapigwa vita ikiwa ukafiri wake unaenea. Ama ikiwa ukafiri wake umefupika kwake, halinganii kwao, hana uchangamfu wowote katika kueneza ukafiri, bali umefupika juu ya nafsi yake, huyu hapigwi vita. Kwa mfano wa wazee makafiri, wanawake, watoto na watawala kwenye masinagogi yao. Hawa hawapigwi vita kwa sababu ukafiri wao umefupika kwao. Kadhalika mwenye kunyenyekea Uislamu na akalipa kodi hapigwi vita. Bali anaachwa juu ya dini yake na inachukuliwa kodi kutoka kwake. Anakuwa ni mwenye kufuata hukumu ya Uislamu. Huyu shari yake imefupika kwake.

Ni jambo linalotambulika kwamba ambaye kodi inachukuliwa kutoka kwake halinganii katika ukafiri. Akiwa atalingania katika ukafiri mkataba wake unavunjika. Ni mwenye kujisalimisha chini ya hukumu ya Kiislamu na analipa kodi katika hali ya unyonge. Huyu ndiye anaachwa. Mtumzima, mtoto na mwanamke ambao ukafiri wao hauvuki kwenda kwa wengine. Kadhalika mtawa ambaye amejitenga na watu na kwenda katika masinagogi yao. Watu aina hii wanaachwa.

Hii ni dalili yenye kuonyesha kuwa dini ya Uislamu sio dini ya mauaji na umwagaji damu. Ni dini ya rehema na uadilifu. Inataka kuwaondosha watu kutoka katika giza kwenda katika nuru kwa ajili ya manufaa yao wao wenyewe. Ni manufaa kiasi gani yamepatikana kwa watu kupitia Jihaad? Wale waliosilimu kutoka katika makafiri kwa wale wasiokuwa waarabu wamesalimishwa na Allaah kutokamana na Moto. Wangeachwa wangelikuwa miongoni mwa watu wa Motoni. Wamesilimu, wakaufanya vizuri Uislamu wao na ndani yao Allaah akawatoa wanachuoni vigogo. Haya ndio matunda ya Jihaad katika njia ya Allaah (´Azza wa Jall). Jihaad ndio nundu ya Uislamu.

[1] 51:56

[2] 02:193

[3] 08:39

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 118-120
  • Imechapishwa: 25/05/2021