Ama kuwaomba msaada wafu ni jambo halijuzu kabisa. Wafu hawawezi kitu. Ni mamoja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala mwenginewe. Wao wako katika ulimwengu na wewe uko katika ulimwengu mwingine. Kwa hiyo usitafute kutoka kwa wafu chochote kwa hoja kwamba wana karama na kwamba wana uwezo, ni batili. Maiti haombwi kitu ijapokuwa ni katika mbora kabisa wa watu.

Vivyo hivyo aliye hai haombwi asichoweza yeyote isipokuwa Allaah. Haombwi jambo la kumponya mgonjwa, kutunuku mtoto au kuleta riziki. Viumbe hawaombwi vitu asivyoweza yeyote isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 115
  • Imechapishwa: 24/05/2021