81. ´Aqiydah ya Ibn ´Abdil-Wahhaab juu ya kumshuhudilia mtu Pepo au Moto

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Simshuhudilii muislamu yeyote Pepo wala Moto isipokuwa ambaye ameshuhudiliwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini namtarajia mema mwema na nachelea khatari juu ya mfanya maovu. Simkufurishi yeyote katika waislamu kwa dhambi na wala simtoi katika mduara ya Uislamu.

MAELEZO

Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwamba hawamshuhudilii Pepo mtu yeyote kwa dhati yake ijapokuwa ni miongoni wa watu wema na wala hawamshuhudilii yeyote Moto ijapokuwa ni miongoni mwa makafiri. Kama kusema “huyu ni miongoni mwa watu wa Peponi au huyu ni miongoni mwa watu wa Motoni.” Kitendo hicho hakijuzu. Isipokuwa yule ambaye Allaah amemfunulia ghaibu; ambaye ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakumfunulia ghaibu yote. Bali amemfunulia sehemu tu katika mambo yaliyofichikana. Katika hayo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewashuhudilia baadhi ya watu Pepo. Hivyo sisi pia tunawashuhudilia kwamba ni katika watu wa Peponi. Kwa mfano wale Maswahabah kumi waliobashiriwa Pepo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); wale makhaliyfah wanne, Twalhah, az-Zubayr bin al-´Awwaam, Sa´d bin Abiy Waqqaas, Sa´iyd bin Zayd, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf na Abu ´Ubaydah ´Aamir bin al-Jarraah. Hawa wameshuhudiliwa Pepo na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile Thaabit bin Qays bin Shammaas ambaye ameshuhudiliwa Pepo na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawa tunawashuhudilia. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewashuhudilia kwa dhati zao. Tunasema kwa mfano fulani yuko Peponi, Abu Bakr yuko Peponi, ´Umar yuko Peponi, Twalhah yuko Peponi, az-Zubayr yuko Peponi na hawa wengine wako Peponi kwa sababu Mtume ameeleza kuwa wako Peponi.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hazungumzi kwa matamanio. Ijapokuwa haya ni kwa ma ghaibu lakini Allaah amemfunulia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya ghaibu hiyo:

عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُولٍ

”Mjuzi wa mambo yaliyofichikana na wala hamdhihirishii yeyote ghaibu Yake; isipokuwa yule aliyemridhia ambaye ni Mtume.”[1]

Allaah humfunulia Mtume sehemu katika mambo ya ghaibu kwa ajili ya manufaa ya watu.

[1] 72:26-27

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 116
  • Imechapishwa: 24/05/2021