73. Ni Aayah ipi ya mwisho iliyoteremka kutoka katika Qur-aan?

Swali 73: Ni Aayah ipi ya mwisho iliyoteremka kutoka katika Qur-aan?

Jibu: Kwa mujibu wa al-Baraa´ bin ´Aazib ilikuwa:

يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ

”Wanakuuliza hukumu ya Shari´ah. Sema: ”Allaah anakubainishieni kuhusu a asiye na watoto wala mzazi.”[1]

Kwa mujibu wa ´Umar Aayah ya mwisho kuteremshwa ilikuwa kuhusu ribaa.

Kwa mujibu wa Ibn Shihaab Aayah ya ribaa na Aayah ya deni ndio zilikuwa za mwisho kuteremka. Ibn ´Abbaas amesema:

”Cha mwisho kuteremshwa kutoka katika Qur-aan ilikuwa:

وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّـهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ

”Iogopeni Siku mtakayorejeshwa kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa kamilifu iliyoyachuma, nao hawatodhulumiwa.”[2]

Hayohayo ndio yamesemwa na Abu Sa´iyd al-Khudriy. Ibn ´Abbaas amesema:

”Iliteremshwa siku kumi na tatu kabla ya kifo chake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Sa´iyd bin Jubayr amesema mfano wa hayo kuhusu Aayah ya mwisho na akaongeza:

”Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliishi siku tisa baada ya kushushwa kwake. Kisha akafariki  jumatatu wakati kumebakia siku mbili za Rabiy´ al-Awwal.”[3]

Huenda mwanzoni mwa Aayah ya ribaa hadi mwisho wa Aayah ya deni zilishushwa kwa pamoja – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[1] 4:176

[2] 2:281

[3] Tafsiyr Ibn Abiy Haatim (2/554).

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 144
  • Imechapishwa: 08/11/2023