Kuchinja:

1 – Raafiy´ bin Khadiyj amesema:

”Ee Mtume wa Allaah! Hakika kesho tutakutana na adui na hatuna visu.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Kuleni katika kile ambacho imemwagika damu yake na kutajiwa jina la Allaah – lakini si kwa jino na kucha. Nitakueleza; jino ni mfupa na kucha ni kisu cha Wahabeshi.”[1]

[1] al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, at-Tirmidhiy, Ibn Maajah, al-Bayhaqiy, Ahmad na at-Twahaawiy katika ”Sharh-ul-Ma´aaniy”.

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuchinja kwa kucha kwa kutoa sababu kuwa ni mfumo wa Wahabeshi na kwamba meno ni mfupa. Wanazuoni wametofautiana juu ya sababu hiyo. Watu wa maoni (أهل الرأي) wameona kuwa kuchinja kwa kucha na jino ni kwa sababu kunafanana na kunyonga au kunapelekea kunyonga – mnyama aliyenyongwa ameharamishwa kumla. Hata hivyo wanaruhusu zana kama hizo za uchinjaji ikiwa uchinjaji ni kwa kutumia vitu vilivyonolewa vizuri. Kwa sababu kuchinja kwa zana zilizotenganishwa na kunolewa hakuhesabiwi kama kunyonga.

Kikosi kikubwa cha wanazuoni wamekataza hilo kwa hali zote. Hoja yake ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alibagua jino na kucha miongoni mwa zile zana za kuchinjia. Kwa hiyo ikatambulika kuwa hivyo ni vifaa vilivyonolewa ambavyo haijuzu kuvitumia katika kuchinja. Vingelikuwa vinanyonga basi asingevibagua. Dhana inazingatiwa kama uhalisia ikiwa sababu imefichwa au haikupangwa, hapana endapo iko dhahiri na imepangwa. Isitoshe hoja hiyo inapingana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ”… kucha ni kisu cha Wahabeshi” kunapelekea kwamba kuna athari katika makatazo haya. Ima sababu yenyewe ndio ikawa matatizo, dalili juu ya makatazo au sifa moja wapo ya sababu au dalili yake. Wahabeshi kucha zao ni refu na ndio watu pekee wanaochinja kwa kutumia kucha zao. Kwa hiyo kuna uwezekano makatazo yanatokana na kujifananisha nao kwa sababu kitendo hicho kinafanywa na watu peke yao.” (Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 54-55)

Haafidhw Ibn Hajar amesema:

”Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ”… kucha ni kisu cha Wahabeshi” yanasisitiza kwamba walikuwa makafiri na tumekatazwa kujifananisha na wao, ndivo alivosema Ibn-us-Swalaah na an-Nawawiy. Amepingwa kwamba mambo yangelikuwa hivo basi visu pia vingelikatazwa kwa sababu makafiri pia hutumia visu na vyenginevyo. Jawabu langu ni kwamba kuchinja kwa kisu ndio msingi. Vyengine vyote ndivo vinaambatanishwa na kujifananisha. Kwa ajili hiyo ndio maana walikuwa wakiuliza kama inafaa kuchinja kwa kitu kingine kisichokuwa kisu.” (Fath-ul-Baariy)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 181-182
  • Imechapishwa: 08/11/2023