71. Maana ya kumswalia na kumtakia amani Mtume

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

“Allaah kumswalia mja Wake ni kule kumsifu katika ulimwengu wa juu.”

Kwa hiyo wewe unaposema:

“Ee Allaah! Mswalie Muhamamd.”

unakuwa umemwomba Allaah (Ta´ala) amsifu mja Wake katika ulimwengu wa juu ambao ni Malaika. Kama alivyosema al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake kutoka kwa Abul-´Aaliyah aliyesema:

“Allaah kumswalia mja Wake ni kule kumsifu katika ulimwengu wa juu.”[1]

Maneno yake:

“Imesemekana vilevile kwamba ni rehema.”[2]

Maana yake inakuwa:

“Ee Allaah! Mrehemu Muhammad!”

Maneno yake:

“…. lakini ya kwanza ndio sahihi zaidi.”

Hii ndio sahihi zaidi iliyosemwa maana ya Allaah kumswalia mja Wake[3].

Maneno yake:

“Ama kuhusiana na kwamba Malaika pia wanafanya hivyo, maana yake ni kwamba wanamwombea msamaha… “

Malaika wanapomswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maana yake ni kumuombea msamaha.

Maneno yake:

“… na kwamba wanaadamu wanafanya hivyo, maana yake ni du´aa.”

Wanadamu wanapomswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maana yake ni kumuombea du´aa.

Allaah anapomswalia mja Wake ni kumsifu katika ulimwengu wa juu. Malaika wanapomswalia ni kumuombea msamaha. Wanadamu wanapomswalia ni kumuombea du´aa.

Maneno yake:

“Mbariki… “

Bi maana sema:

و بارك على محمد و على آل محمد

“Na mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad.”

Maneno yake:

“Yanayokuja baada yake, yanazingatiwa kuwa ni katika maneno na matendo yaliyopendekezwa.”

Anayesema:

التحيات لله

“Maadhimisho yote yanamstahikia Allaah.“

Mpaka:

اللهم صل على محمد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad.“

Akasema:

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na baraka za Allaah ziwe juu yenu.”

atakuwa amefanya mambo ya wajibu. Kuhusu ambaye atazidisha juu ya hayo katika kuomba baraka, Tawarruk na mengineyo basi ima ni mambo yaliyopendekezwa ya kimaneno au kivitendo.

[1] al-Bukhaariy (04/1802) ikiwa na cheni pungufu kwa tamko la kukata. al-Qaadhwiy Abu Ishaaq ameiunganisha katika ”Fadhwl-us-Swalaati ´alaan-Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)” nambari. 95.

[2] Jalaa´-ul-Afhaam, uk. 158 ya Ibn-ul-Qayyim.

[3] Fath-ul-Baariy (11/156).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 102-103
  • Imechapishwa: 30/06/2022