69. Muqtadha ya kushuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah

Ni lazima yapatikane mambo haya wakati wa kushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah:

1- Kutamka kwa ulimi.

2- Kuamini ndani ya moyo.

3- Kumfuata yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Haitoshi kwa mtu kutambua kwamba ni Mtume wa Allaah na akatamka jambo hilo lakini asimfuate, asimtii katika aliyoamrisha na wala asijiepushe aliyomkataza na akamkadhibisha katika aliyoelezea. Kwa ajili hiyo amesema Shaykh katika ibara nzuri katika “Thalaathat-ul-Usuwl”:

“Maana ya “nashuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah” ni kumtii katika yale aliyoamrisha, kumsadikisha katika yale aliyoelezea, kujiepusha na yale aliyokataza na kugombeza na kutoabudiwa Allaah isipokuwa na kwa yale aliyoweka katika Shari´ah.”

Midhali mja anashuhudia kwamba ndiye Mtume wa Allaah basi ni lazima ajifungamanishe na yale aliyokuja nayo na wala asimkhalifu kwa Bid´ah na mambo yanayokwenda kinyume.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 17/05/2021