69. Radd kwa anayedai ya kwamba mwenye kutimiza nguzo za Uislamu hawezi kuwa kafiri

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mlango wa kumi na mbili

Radd kwa anayedai ya kwamba mwenye kutimiza nguzo za Uislamu hawezi kuwa kafiri

Ukihakikisha [elewa] ya kwamba wale aliyowapiga vita Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa na akili nzuri na shirki kidogo kuliko watu hawa, basi jua kuwa hawa wana shubuha wanayoitaja. Hoja tata hii tumeshaitaja na ni katika hoja zao tata kubwa. Hivyo sikiliza vizuri majibu yake. Wanasema:

“Wale ambao Qur-aan iliwateremkia walikuwa hawashuhudii ya kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah, na walikuwa wanamkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanapinga kufufuliwa, wanakadhibisha Qur-aan na kuiona kuwa ni uchawi. Lakini sisi tunashuhudia ya kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, tunaisadikisha Qur-aan, tunaamini kufufuliwa, tunaswali na tunafunga. Vipi basi mtatufanya sisi ni kama wao?””

MAELEZO

Hapa (Rahimahu Allaah) anabainisha hoja yao tata kubwa. Ameiraddi na kusema:

“Ukielewa ya kwamba wale aliyowapiga vita Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa na akili nzur… “

Hii ni hoja tata kubwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 80
  • Imechapishwa: 25/11/2023