68. Washirikina wa leo wanaomba pamoja na Allaah watenda madhambi

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

2 – Watu wa mwanzo walikuwa wakiomba pamoja na Allaah watu waliokuwa karibu na Allaah. Ima Mitume, mawalii au Malaika. Walikuwa wakiomba miti au mawe vinavyomtii Allaah na havimuasi. Ama watu wa zama zetu wanaomba pamoja na Allaah katika watenda madhambi wakubwa. Na wale wanaowaomba ndio wanaowahalalishia maovu kama zinaa, kuiba, kuacha swalah na mengineyo.

Yule anayemuamini mtu mwema au yule ambaye haasi, kama mfano wa mti na jiwe, ni uovu kidogo kuliko yule anayemuamini yule anayeshuhudia anafanya madhambi na ufisadi na akathibitisha hilo.

MAELEZO

Jambo la pili lenye kubainisha kuwa mshirikina wa zama zake (Rahimahu Allaah) alikuwa ni mbaya zaidi kuliko mshirikina wa zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ni kwamba walikuwa ima wakiwaomba Mawalii wa Allaah (´Azza wa Jall) au wakiyaomba mawe na miti vinavyomtii Allaah. Upande mwingine washirikina wa zama zake walikuwa wakiwaomba watu wanaotuhumiwa madhambi, uzinzi, kuiba na matendo mengine ya maasi. Ni jambo lenye kujulikana kuwa yule mwenye kumuamini mtu ambaye madhambi yake yako waziwazi ni mbaya zaidi kuliko yule anayemwamini mtu mwema au kitu kisichokuwa na uhai ambacho hakimuasi Allaah (Ta´ala). Hili ni jambo liko wazi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 80
  • Imechapishwa: 25/11/2023