Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Hii ndio maana ya “hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah”.

Katika Hadiyth:

“Kichwa cha mambo ni Uislamu, nguzo yake ni swalah na Jihaad katika njia ya Allaah ndio nundu yake ya juu.”[1]

Allaah ndiye anajua zaidi. Swalah na amani ziwe juu ya Muhammad, familia yake na Maswahabah zake.

MAELEZO

Bi maana kichwa cha Uislamu ni Tawhiyd aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); kumshuhudilia Allaah upwekekaji na kumshuhudilia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Ujumbe. Nguzo yake ni swalah ambayo ni nguzo kubwa. Nundu yake ni kupambana jihaad katika njia ya Allaah.

Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.

[1] Ahmad (5/231-237), at-Tirmidhiy (5/13) na Ibn Maajah (2/1394).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 111
  • Imechapishwa: 19/02/2023