66. Radd juu ya shubuha wanayotumia Mu´tazilah na vifaranga vyao kupinga kuonekana kwa Allaah Aakhirah II

Shubuh ya pili: Wameshikilia udhahiri wa maneno Yake (Ta´ala):

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki.”[1]

Wamesema kuwa maana ya kudiriki ni kwamba hawatomuona. Tunaraddi kwa kusema kwamba maana ya:

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki.”

maana yake si kuwa hayamuoni. Lakini maana yake ni kwamba hayamzunguki. Maana ya kudiriki ni kukizunguka kitu. Allaah hakusema:

لا تراه الأبصار

“Macho hayamuoni.”

Bali amesema:

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki.”

Kukanushwa uzuungukaji hakupelekei kukanushwa uonekanaji. Mtu anaweza kukiona kitu lakini asikizunguke chote. Kwa mfano wewe unaliona jua lakini si kwamba unalizunguka lote katika kuliona. Si kila chenye kuonekana kinazungukwa chote. Kwa hiyo Aayah haipingi kuonekana kwa Allaah. Bali inapinga uzungukaji ijapokuwa yanamuona lakini hayawezi kumzunguka. Yakimuona hayamzunguki. Kwa sababu Allaah (Jalla wa ´Alaa) ni mkubwa zaidi kuliko kila kitu. Kwa hiyo hazungukwi (Jalla wa ´Alaa). Kwa hiyo katika Aayah hakuna dalili inayopinga kuonekana kwa Allaah. Kilichopingwa ni uzungukaji.

[1] 06:103

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 95-96
  • Imechapishwa: 17/05/2021