66. Kufaa kukusanya kunapopatikana sababu yake

Swali 66: Je, nia ni sharti ya kufaa kukusanya? Inatokea mara nyingi watu wanaswali mkusanyiko wa Maghrib pasi na nia ya kukusanya na baada ya swalah ya Maghrib waswaliji wanashauriana kisha wanaswali ´Ishaa?

Jibu: Wanazuoni wametofautiana juu ya jambo hilo. Maoni yaliyo na nguvu ni kwamba nia sio sharti wakati wa kufungua swalah ya kwanza. Bali inafaa kukusanya baada ya kumaliza kuswali swalah ya kwanza kukipatikana sharti yake ambayo ni khofu, maradhi au mvua.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 70
  • Imechapishwa: 12/09/2022