64. Je, safari inayomruhusu mtu kufupisha swalah imewekewa kikomo cha umbali maalum?

Swali 64: Unasemaje juu ya safari inayomruhusu mtu kufupisha swalah imewekewa kikomo cha umbali maalum? Unaonaje juu ya ambaye amenuia katika safari yake kukaa zaidi ya siku nne anaruhusiwa kufupisha[1]?

Jibu: Wanazuoni wengi wanaona kuwa imewekewa kikomo cha umbali wa mchana mmoja na usiku wake kwa mwendo wa ngamia na mwendo wa kawaida wa kutembea kwa miguu, jambo ambalo ni karibu 80 km. Kwa sababu umbali huu kidesturi ndio unazingatiwa kuwa safari tofauti na umbali chini ya hapo.

Kikosi cha wanazuoni wengi wanaona kuwa ambaye ameamua kukaa zaidi ya siku nne basi atalazimika kuswali kwa kukamilisha na kufunga katika Ramadhaan. Muda ikiwa ni chini ya hapo basi inafaa kwake kufupisha, kukusanya na kuacha kufunga. Kwani msingi juu ya mkazi ni kuswali kwa kukamilisha. Imesuniwa kwake kufupisha pale anaposafiri.

Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba katika hajj ya kuaga aliikaa siku nne hali ya kuwa ni mwenye kufupisha swalah. Kisha akasafiri kwenda Minaa na ´Arafah. Kwa hiyo hayo yakafahamisha kufaa kufupisha kwa ambaye ameazimia kukaa siku zisizozidi nne.

Kuhusu kukaa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku kumi na tisa mwaka wa Ufunguzi na siku ishirini Tabuuk ni yenye kufasiriwa kwamba hakukusanya kwa sababu ya ule ukaazi. Aliikaa kutokana na sababu ambayo hakuwa anajua itaishi lini. Hivi ndivo walivyooanisha kikosi cha wanazuoni wengi kule kukaa kwake Makkah mwaka wa Ufunguzi na Tabuuk mwaka wa vita vya Tabuuk kwa ajili ya kuchukua tahadhari katika dini na kutendea kazi ule msingi ambao; ulazima wa kuswali nne kwa ambao ni wakazi inapokuja katika Dhuhr, ´Aswr na ´Ishaa.

Lakini akiwa hakunuia kukaa bali hajui ni lini atasafiri, huyu anaruhusiwa kukusanya na kufupisha swalah mpaka pale atakaponuia kukaa zaidi ya siku nne au akarejea katika mji wake.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/270-271).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 68
  • Imechapishwa: 12/09/2022