Swali: Hadiyth inayosema:

“Watu aina saba Allaah atawafunika chini ya kivuli Chake.”

Ziada inayosema:

“Watu aina saba Allaah atawafunika chini ya kivuli cha ´Arshi Yake.”

Ni Swahiyh?

Jibu: Ndio.

Swali: Wale ambao wamedhoofisha ziada hiyo wana haki ya kusema kuwa ambaye atasema chini ya kivuli cha ´Arshi Yake amepindisha maana? Je, ambaye amesema kuwa ni kivuli ambacho Allaah atakiumba siku hiyo anayo hoja juu ya maoni hayo?

Jibu: Kwa hali yoyote mambo kama haya mtu anatakiwa kukomeka juu ya yale yaliyopokelewa. Muda wa kuwa kumethibiti kivuli cha Allaah (Jalla wa ´Alaa) basi kinatakiwa kuthibitishwa kutokana na inavyolingana na utukufu na  ukubwa Wake. Kuhusu kivuli cha Allaah hakilingani na vivuli vya viumbe Wake. Hakuna mgongano kati ya vivuli hivyo viwili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Kariym bin ´Abdillaah al-Khudhwayr
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://saif.af.org.sa/sites/default/files/02_32.mp3
  • Imechapishwa: 12/09/2022