Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Wa mwanzo wao alikuwa ni Nuuh (´alayhis-Salaam) na wa mwisho wao alikuwa ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Dalili juu ya kwamba wa mwanzo wao alikuwa ni Nuuh (´alayhis-Salaam) ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ

”Hakika Tumekuletea Wahy kama tulivyomletea Nuuh na Manabii baada yake.”[1]

Allaah ameutumia kila ummah Mtume, kuanzia kwa Nuuh mpaka kwa Muhammad, ili kuwaamrisha kumuabudu Allaah peke Yake na akiwakataza shirki. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut.””[2]

Allaah amewafaradhishia viumbe vyote kukanusha Twaaghuut na badala yake kumuamini Allaah. 

MAELEZO

Nuuh ndio Mtume wa kwanza aliyetumilizwa na Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) kwa watu wa ardhini baada ya kutokea shirki. Allaah alimtuma kwa wanawe na wengineo. Lakini alitanguliwa na Nabii; naye ni Aadam (´alayhis-Salaam) ambaye alikuwa Nabii kati ya dhuriya yake. Hata hivyo shirki haikutokea katika zama zao. Kilichotokea ni maasi peke yake. Qaabiyl alimuua ndugu yake Haabiyl. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

وَمَا كَانَ النَّاسُ إِلَّا أُمَّةً وَاحِدَةً فَاخْتَلَفُوا ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ فِيمَا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ

”Wala watu hawakuwa isipokuwa ni ummah mmoja kisha wakatofautiana. Na kama si neno lililotangulia kutoka kwa Mola wako,  basi bila shaka ingehukumiwa kati yao katika yale waliyokuwa kwayo wakitofautiana.”[3]

Baina ya Aadam na Nuuh kulipita karne kumi. Wote walikuwa wakimwabudu Allaah pekee. Kisha shirki ikajitokeza kati ya watu wa Nuuh. Wakafa watu wema katika zama za Nuuh akiwemo Wadd, Suwaa´, Yaghuuth, Ya´uuq wa Nasr kwa muda wa karibu. Wakahuzunika na wakatengeneza picha zao ili waweze kukumbuka ´ibaadah zao ili ziwafanye kupata uchangamfu. Baadaye wakaja wajukuu zao wakawaabudu. Ibliys aliwadanganya na akawaambia:

“Babu zenu walikuwa wakiomba mvua kupitia wao” na hivyo wakawaabudu. Hapo ndipo   Allaah alimtumiliza Nuuh baada ya kujitokeza kwa shirki.”[4]

Vivyo hivyo Aadam alikuwa Mtume kwa wanawe na wale waliokuwa pamoja nao. Kuhusu Nuuh yeye alikuwa Nabii kwa wanawe na wengineo na ndiye Mtume wa kwanza aliyetumilizwa na Allaah baada ya kujitokeza kwa shirki.

Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

”Allaah ameutumia kila ummah Mtume… ”

Allaah ameutumia kila ummah Mtume, kuanzia kwa Nuuh mpaka kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam) wakiwaamrisha kumwabudu Allaah pekee na wakiwakataza kuabudu waungu wa batili na shirki na wengineo wasiokuwa Allaah. Twaaghuut ni kila mwenye kuabudiwa badala ya Allaah. Isipokuwa tu wale wasiokuwa radhi kuabudiwa badala ya Allaah kama vile Mitume na ´Iysaa hawatakiwi kuitwa ´Twaaghuut`.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

”Allaah amewafaradhishia viumbe vyote kukanusha Twaaghuut… ”

Kukufuru Twaaghuut ni kujitenga mbali na kila chenye kuabudiwa badala ya Allaah, kukiacha, kukifanyia uadui, kukichukia, kuwachukia watu wake na uamini ubatilifu wa kuabudiwa asiyekuwa Allaah, akiepuke, akikemee, kuwakafirisha watu wake, kuwachukia na kuwafanyia uadui. Hilo ni faradhi kwa kila muislamu. Amesema (Ta´ala):

فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٌٰ

”Basi atakayemkanusha twaaghuut na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti.”[5]

Neno la Tawhiyd limekusanya sehemy hizo mbili; ndani yake kuna kukufuru Twaaghuut ambako ni ´hapana mungu wa haki` na ndani yake kuna kumuamini Allaah ambako ni ”isipokuwa Allaah”.

[1] 04:163

[2] 16:36

[3] 10:19

[4] Tazama ”Tafsiyr Ibn Jariyr” (02/275, 23/639) na ”ad-Durar al-Manthuur” (08/293-295).

[5] 02:256

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 107-108
  • Imechapishwa: 19/02/2023