3 – Anas amesema kuhusu vita vya Khaybar wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimchagua Swafiyyah kuwa mke wake:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliondoka kwenda Khaybar na hakulala naye usiku uliopita. Wakati alipoletwa ngamia mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili aondoke, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuwekea Swafiyyah mguu wake ili aweke mguu wake juu ya paja lake. Akakataa na akaweka goti lake juu ya paji lake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamfunika na akambeba nyuma yake. Baada ya hapo akaweka shuka juu ya mgongo wake na uso wake kisha akaifunga chini ya mguu wake na kumfanya sawa na wake zake wengine.”[1]

[1] Ibn Sa´d kupitia njia nyingi, akiwemo pia Abu Hurayrah, Abu Ghatafaan bin Twurayf al-Murriy, Anas bin Maalik na Umm Sinaan al-Aslamiyyah. Ibn Sa´d amesema:

”Masimulizi yao yameingiliana.”

Ameipokea pia al-Bukhaariy, Muslim na wengineo kupitia kwa Anas, kama ilivyokwishatangulia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 104
  • Imechapishwa: 04/10/2023